1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya kuitangazia vita al-Shabaab

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kithure Kindiki, ameapa kuwa nchi yake itaingia kwenye vita kamili dhidi ya kundi la wanamgambo wa al-Shabaab la nchini Somalia.

https://p.dw.com/p/4XhMi
Somalia Militants Twitter
Wanamgambo wa kundi la al-Shabaab.Picha: picture alliance / AP Photo

Kindiki aliwataja watu 35 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi hilo na waliohusika na mashambulizi katika mpaka wa nchi hiyo na Somalia.

Kindiki aidha alisema watu hao wanatafutwa kwa kuhusika na kutega vifaa vya kuripuka katika barabara kadhaa kwenye eneo hilo.

Waziri huyo pia alisema kuwakamata au kuwaua magaidi hao linabaki lengo kuu wanalolifuatilia kwa haraka na hatua nyingine na mikakati mingine imewekwa kuvishinda vita dhidi ya ugaidi.

Soma zaidi: Marekani yatowa dola $5M kumpata kiongozi wa al-Shabaab

Kauli ya Kindiki imefuatiwa na hatua ya Marekani kuahidi zawadi ya kitita cha dola milioni 5 kwa taarifa kumhusu kiongozi wa kundi la al-Shabaab nchini Somalia, Abukar Ali Adan.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema Abukar Ali Adan ambaye alitangazwa rasmi kama gaidi na Marekani mnamo 2018, ni naibu kamanda wa al-Shabaab na anahusishwa na matawi kadhaa ya mtandao wa kigaidi ya al-Qaida.