Khan ahimiza wafuasi wake kufanya maandamano mapya
6 Desemba 2024Hayo yamesemwa na chama chake leo kufuatia maandamano yenye vurugu yaliofanyika wiki iliyopita.
Khan, ambaye amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja, amewataka wafuasi wake wakusanyike mnamo Disemba 13 katika mji wa kaskazini magharibi wa Peshawar, mji mkuu wa jimbo la Khyber-Pakhtunkhwa unaoongozwa na chama chake.
Wito huu wa hivi karibuni ameutoa wiki moja tu baada ya maelfu ya wafuasi wake kuandamana kwa siku nne katika mji mkuu Islamabad huku chama chake kikisema waandamanaji 12 waliuawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano hayo.
Polisi Pakistan yatoa mashtaka mapya dhidi ya Imran Khan na mkewe
Mahakama ya kupambana na ugaidi jana Alhamisi ilimshtaki Khan na wafuasi wake kadhaa kwa tuhuma za kuongoza mashambulizi dhidi ya jeshi mnamo Mei, 2023. Hata hivyo, wamekanusha mashtaka dhidi yao.