1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim ausifu uhusiano unaotanuka wa Korea Kaskazini na Urusi

12 Juni 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un leo ameusifu uhusiano unaozidi kutanuka kati ya nchi yake na Urusi

https://p.dw.com/p/4gwmi
Marais Kim Jong Un na Vladimir Putin nchini Urusi
Marais Kim Jong Un na Vladimir Putin nchini UrusiPicha: Vladimir Smirnov/AFP

Baadhi ya ripoti za vyombo vya habari zinasema huenda ziara hiyo ya Putin ikafanyika wiki ijayo na shirika la habari la Japan, NHK, linasema Putin atafanya ziara Vietnam pia.

NHK linaripoti kuwa, katika ziara hiyo Putin atakuwa anatafuta ushirikiano mkubwa wa kijeshi na Korea Kaskazini kwa kuwa Urusi inakabiliwa na upungufu wa silaha katika vita vyake na Ukraine.

Korea Kaskazini nayo inadaiwa kuwa inataka usaidizi wa teknolojia baada ya kushindwa kuweka setalaiti yake ya pili ya upelelezi katika mzunguko wa dunia, mwishoni mwa mwezi Mei.

Urusi na Korea Kaskazini zote hazijathibitisha taarifa hizo za ziara ya Putin.