1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Milton chaua 10 Florida

11 Oktoba 2024

Kimbunga Milton kinachopiga kwenye jimbo la Florida nchini Marekani kimesababisha hadi sasa vifo vya watu kumi, huku nyumba na maeneo ya biashara yapatayo milioni tatu yakiwa hayana huduma ya umeme.

https://p.dw.com/p/4lepK
Kimbunga Milton Florida
Kimbunga Milton kikisababishia mafuriko Florida.Picha: Joe Raedle/Getty Images

Kimbunga hicho, ambacho mamlaka za hali ya hewa zinasema kimefikia Daraja ya 3, kinatajwa kuwa kikubwa zaidi tangu mwaka 1986.

Mamlaka ya Hali ya Hewa imetowa maonyo 126 ya tufani kwenye jimbo la Florida tangu Jumatano.

Rais Joe Biden amewasihi watu kusalia majumbani mwao na kufuata maelekezo ya wafanyakazi wa huduma za uokozi.

Soma zaidi: Kimbunga Milton chaacha uharibifu mkubwa Florida

Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump, na mkewe Melania, wameonekana kwenye video iliyosambazwa mitandaoni wakiswali kuwaombea watu wa Florida na wakati huo huo wakiomba kura.

Kimbunga Milton kinatokea wiki mbili tu, baada ya Kimbunga Helene kusababisha vifo vya 237 ndani ya jimbo hilo na mengine nchini Marekani.