1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Trami chaua watu wapatao 100 nchini Ufilipino

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Waokoaji nchini Ufilipino wanaendelea na zoezi la kupiga mbizi kwenye ziwa na kuzunguka vijiji vilivyotengwa ili kuwatafuta watu ambao wamepotea, wakati idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Trami vikifikia 100.

https://p.dw.com/p/4mHSk
Athari za kimbunga Trami Ufilipino
Athari za kimbunga Trami UfilipinoPicha: Philippine Coast Guard via AP/picture alliance

Waokoaji nchini Ufilipino wanaendelea na zoezi la kupiga mbizi kwenye ziwa na kuzunguka vijiji vilivyotengwa leo Jumapili ili kuwatafuta watu ambao wamepotea, wakati idadi ya vifo vilivyotokana na kimbunga Trami vikifikia 100.

Kimbunga Trami ambacho kiliipiga Ufilipino tangu siku ya Alhamis wiki hii, ni miongoni mwa vimbunga vibaya kuikumba nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia mwaka huu. Kwa mujibu wa Ofisi ya taifa inayohusika na maafa, kimbunga hicho kimesababisha zaidi ya watu nusu milioni kukimbia makazi yao na takriban 36 hawajulikani walipo hadi kufikia sasa.

Soma: Idadi ya waliokufa kufuatia kimbunga Gaemi huko Ufilipino yaongezeka na kufikia 33

Watu wamelazimika kuyakimbia makazi yao kutokana na mafuriko, ambayo yamezamisha mamia ya vijiji katika maeneo ya kaskazini mwa Ufilipino.