Tanzania ni moja kati ya nchi zinazozalisha kwa wingi zao la korosho duniani baada ya Ivory Coast, Cambodia, Vietnam na India. Serikali inapania kuongeza uzalishaji wa korosho kufikia tani milioni moja ifikapo mwaka 2030. Je, serikali imeweka mikakati gani kuendeleza zao la korosho? Salma Mkalibala amezungumza na Mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania, Francis Alfred.