Hali ya kisiasa Korea Kusini bado ni tete
6 Desemba 2024Matangazo
Lee amesema bado kuna uwezekano wa Rais Yoon Suk Yeol kutoa tangazo lengine la sheria ya kijeshi ili kujaribu kubadili masaibu yanayomkabili, japo hakutoa ushahidi kuthibitisha madai yake.
Tangazo la Rais Yoon mnamo siku ya Jumanne liliitikisa nchi hiyo yenye uchumi wanne kwa ukubwa barani Asia, huku chama cha Lee cha Democratic na vyama vingine vidogo vikishinikiza kupitisha hoja ya kumshtaki na kumuondoa madarakani Yoon kesho Jumamosi.
Chama tawala chamkosoa Rais wa Korea Kusini
Hoja ya kumuondoa madarakani kiongozi huyo wa Korea Kusini inahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya bunge lenye viti 300, ikimaanisha kuwa angalau wabunge wanane kati ya 108 kutoka chama tawala cha Yoon cha PPP lazime wapige kura kuunga mkono hoja hiyo.