Kiongozi wa upinzani Msumbiji aitisha maandamano mengine
12 Novemba 2024Matangazo
Chama hicho kimekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mwaka 1975 kutoka Ureno.
Mondlane, aliyeshinda kwa asilimia 20 katika uchaguzi wa Oktoba 9 kwa mujibu wa mamlaka inayosimamia uchaguzi, anadai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu. Maandamano ya kupinga matokeo hayo tayari yamegharimu maisha ya watu 30, kulinga na shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch.
Upinzani Msumbiji waitisha maandamano mapya
Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, kiongozi huyo wa upinzani aliandika kwamba watatatiza shughuli zote kuanzia kesho Jumatano hadi Ijumaa kupitia maandamano. Amewarai wafuasi na waandamanaji katika mji mkuu wa Maputo, miji mikuu ya mikoa na mipaka kujitokeza katika maandamano ya wiki hii.