1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMsumbiji

Kiongozi wa upinzani Msumbuji asema polisi wanahimiza vurugu

26 Desemba 2024

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Msumbiji Venancio Mondlane amevituhumu vikosi vya usalama kwa kuhimiza vitendo vya uporaji na vurugu ili kukiruhusu chama tawala kutangaza hali ya dharura baada ya uchaguzi tata.

https://p.dw.com/p/4oawt
Ghasia za uchaguzi Msumbiji
Mashirika ya kiraia yanasema watu 150 wameuawa nchini Msumbiji mpaka sasa Picha: AMILTON NEVES/AFP

Mondlane amesema kwenye mitandao ya kijamii kuwa maandamano yao yanalilenga Baraza la Kikatiba, tume ya uchaguzi na chama cha Frelimo chenyewe, taasisi ambazo anasema zilihusika na udanganyifu.

Amesema hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na polisi dhidi ya waporaji, akiongeza kuwa ni kama wanawahimiza watu kushambulia na kuiba.

Soma pia: Baraza la katiba Msumbiji yathibitsiha ushindi wa chama tawala cha Frelimo

Mahakama ya Kikatiba ya nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika ilithibitisha Jumatatu kuwa Frelimo, ambao wamekuwa madarakani tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka wa 1975, walishinda uchaguzi wa rais Oktoba 9 ambao ulizusha machafuko. Mashirika ya kiraia yanasema watu 150 wameuawa mpaka sasa. Hapo jana, wafungwa 1,000 walitumia fursa ya ghasia hizo na kutoroka jela moja la ulinzi mkali mjini Maputo.