1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano kubwa juu ya hali ya hewa kufunguliwa Colombia

21 Oktoba 2024

Mkutano mkubwa kabisa duniani juu ya viumbe asilia unatarajiwa kuanza nchini Colombia huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizitaka nchi wanachama kubadilisha maneno kuwa vitendo.

https://p.dw.com/p/4m1v0
Mkutano wa COP16 mjini Cali
Wajumbe wanaoshiriki mkutano wa mazingira mjini Cali-ColombiaPicha: Fernando Vergara/AP/dpa/picture alliance

Mkutano mkubwa kabisa duniani juu ya viumbe asilia unatarajiwa kuanza nchini Colombia huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizitaka nchi wanachama kubadilisha maneno kuwa vitendo na kulipa katika mfuko ulioanzishwa ili kuyatekeleza malengo ya kurejesha uhai anuai hadi ifikapo 2030. Wajumbe kushiriki kongamano la mazingira la Colombia

Miaka miwili iliyopita, nchi karibu 200 ziliazimia mjini Montreal, Canada, kuyafikia malengo 23 hadi ufikapo mwaka 2030. Pamoja na mambo mengine, nchi hizo zilikubaliana kulinda angalau asilimia 30 ya ardhi na maeneo ya baharini duniani.

Waziri wa Mazingira wa Ujerumani, Steffi Lemke, amekiri kwamba "hali haijaimarika katika kipindi cha miaka miwili iliyopita." Amesema dunia inahitaji kuelewa jinsi migogoro ya uhai anuwai na hali ya hewa inavyoambatana.