Kongamano la uwekezaji lafunguliwa mjini Berlin
20 Novemba 2023Mkutano huo ulioanza leo ni sehemu ya dhamira ya serikali kuziunga mkono nchi za Kiafrika katika kupata mafanikio ya kiuchumi.
Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck anahudhuria mkutano huo wa kilele, pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, viongozi kumi wa mataifa ya Afrika na serikali, na zaidi ya mawaziri 30 kutoka barani humo.
Soma pia:Mkutano wa uwekezaji Afrika wafanyika Berlin
Heiko Schwiderowski, mkuu wa Chama cha wenye Viwanda na Biashara cha Ujerumani anayehusika namasuala ya kanda ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, DIHK amesema kongamano hilo la uwekezaji lenye wajumbe 800 linaelezewa kuwa kongamano kubwa kabisa la kibiashara kuwahi kufanyika kwenye ardhi ya Ujerumani.
Schwiderowski anasema viongozi wa kibiashara na kisiasa nchini Ujerumani wanatuma ishara muhimu, akiongeza kuwa kupanua mahusiano ya kiuchumi ni jitihada yenye manufaa.