1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini haijajibiwa juu ya msaada kwa Korea Kaskazini

2 Agosti 2024

Korea Kusini imesema leo kuwa haijapokea jawabu lolote baada ya kuwasiliana na Korea Kaskazini kwa ajili ya kutoa msaada wa kiutu kufuatia ripoti za vifo na uharibifu mkubwa uliosababishwa na mafuriko ya hivi majuzi.

https://p.dw.com/p/4j35N
Mafuriko Koresa Kaskazini
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akitembelea eneo lililoathiriwa na mafuriko karibu na mpaka na China, katika Mkoa wa Pyongan KaskaziniJulai 31, 2024.Picha: KCNA/REUTERS

Naibu msemaji wa wizara ya muungano ya Korea Kusini, Kim In-ae, amewaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini iko tayari kutoa msaada wa dharura wa kiutu kwa wahanga wa mafuriko hayo. Mapema wiki hii, Korea Kaskazini ilisema mvua kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa nchini humo zilinyesha katika eneo la mpaka wake wa kaskazini karibu na China, na kusababisha mzozo mkubwa ambapo zaidi ya watu elfu 5 walitengwa katika eneo hilo ambalo hukumbwa na mafuriko mara kwa mara. Kituo cha kitaifa cha habari Korea Kaskazini kiliripoti juzi Jumatano kuwa kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un ameahidi kuwaadhibu vikali maafisa waliozembea katika majukumu yao ya kuzuia majanga na kusababisha vifo vya watu. Ripoti moja ya kituo cha televisheni cha Korea Kusini TV Chosun, imesema kuwa mamia ya watu wamefariki dunia.