Kufuatilia mgawanyiko wa mji wa Berlin
Mnamo Novemba 9, 1989 mpaka wa Mashariki na Magharibi ulifunguliwa ghafla. Usiku huo watu walisherehekea nje ya lango la Brandenburg. Ukuta huo ukageuka historia. DW inafuatilia mabaki ya ukuta ulioitenganisha Berlin.
Lango la Brandenburg
Kuanzia Agosti mwaka 1961 hadi Novemba 1989, Ukuta wa Berlin uliigawa Berlin kwa miaka 28 miezi miwili na siku 27. Lango hilo kwa muda mrefu lilikuwa ishara ya utengano Ujerumani. Hata baada ya ukuta huo kuanguka, hapakuwa na kivuko. Lakini hilo lilibadilika terehe 22 Disemba 1989 kuanzia wakati huo watu wa Berlin wamekuwa wakitembea bila usumbufu katika mji huo.
Kumbukumbu za picha kwa upande wa Mashariki
Picha za kumbukumbu hiyo katika mto Friedrichshain zipo katika ukuta ulio na urefu wa kilomita moja unaoitwa ukuta wa ndani ambako wasanii kutoka kote duniani waliuchora mwaka 1990. Eneo hilo kwa sasa linavutia watalii wengi kutoka kote dunian, lakini baadhi ya shemu za kuta hizo zimetolewa kama sehemu ya ujenzi upya.
Kumbukumbu ya Ukuta wa Berlin
Hapana mahala palipo na kumbukumbu ya ukanda wa mauti kama hapa. Ukuta ulio na urefu wa mita 80 umekarabatiwa upya eneo hili linaashirikia utengano wa Ujerumani na una majina ya watu walioangamia au kuuawa katika ukuta wa Berlin.
Ufuatiliaji wa chanzo cha ukuta
Ukuta wa Berlin umetoweka karibu kila mahali mjini humo. Upande wa Mashariki na Magharibi umekuwa kwa pamoja. Katika eneo la barabara ilioko mjini kuna alama zinazoashiria mahala ukuta ulipooitia.
Kituo cha ukaguzi cha Charlie
Hiki kivuko hapa ni miongoni mwa maeneo maarufu mjini Berlin. Wageni na wanadiplomasia pekee ndio walioruhusiwa kupitia hapa. Oktoba 1961, muda mfupi baada ya kujengwa ukuta huo kulikuwa na mgogoro kati ya wanajeshi wa kisovieti na majeshi ya Marekani kwa kusogeleana ana kwa ana.
Kasri la Machozi
Hapa ndipo palikuwa mahali pa kuagana palipojaa vilio vya huzuni. Maelfu kwa maelfu ya watu walipitia hapa katika kituo Friedrichstrasse walipokuwa wanaondoka Ujerumani Mashariki kuelekea Magharibi mwa Berlin. Eneo hili sasa linatumika kama kumbukumbu ya namna kulivyokuwa na utengano wa lazima kwa marafiki na familia.
Kumbukumbu ya Hohenschönhausen
Jela hii imekuwa kumbukumbu kwa wafungwa wa utawala wa kidikteta wa kikomunisti tangu mwaka 1994. Wanaoitembelea wanafahamishwa kuhusu hali ya kizuizini, na njia za kuhojiwa uliofanywa na utawala huo mashariki mwa Ujerumani.
Kituo cha usikivu cha Teufelsberg
Baada ya vita vya kwanza vya dunia, eneo hili lilitumika kutupia uchafu, vifusi vya vita hivyo viliokotwa na kuundwa Teufelsberg, muinuko mrefu zaidi mjini Berlin. Wakati wa vita baridi shirika la ujasusi la Marekani lilitumia eneo hilo kama kituo cha kusikilizia na kudhibiti mawasiliano ya radio.
Makumbusho ya upelelezi Ujerumani
Makumbusho hii karibu na barabara ya Potsdamer Platz inawapeleka wageni katika ulimwengu wa udukuzi. ukiangazia hasa shughuli zilizokuwa zikifanyika wakati wa vita baridi mjini Berlin. Miongoni mwa maonyesho 300 yaliyopo ni gari kutoka Ujerumani Mashariki lililokuwa na camera zilizofichwa katika milango yake.
Njia ya ukuta wa Berlin
Ukuta wa Berlin unafuata mkururo wa mgawanyiko wa zamani wa mji na una urefu wa karibu kilomita 160. Japan ilitoa miti 10,000 ya mcheri ili kuleta amani katika nyoyo za watu. Miche hiyo ilipandwa katika maeneo tofauti ya ukuta wa zamani.