1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah lavishambulia vikosi vya Israel nchini Lebanon

Angela Mdungu
20 Oktoba 2024

Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran limesema limevurumisha mkururo wa maroketi yaliyowalenga wanajeshi wa Israel mapema Jumapili karibu na mpaka huko kusini mwa Lebanon.

https://p.dw.com/p/4m0Mp
Beirut, Lebanon
Moshi ukifuka katika moja ya mashambulizi ya Israel dhidi ya kundi la Hezbollah nchini LebanonPicha: ANWAR AMRO/AFP

Hezbollah limesema mashambulizi yake dhidi ya adui, yalielekezwa nje kidogo mwa kijiji cha Markaba pamoja na kijiji cha Adaisseh. Nalo jeshi la Lebanon limearifu kuwa wanajeshi wake watatu wameuwawa katika shambulio lililofanywa na Israel lililolilenga gari la wanajeshi hao. Waliuwawa wakiwa katika Barabara inayoviunganisha vijiji vya Ain Ebel na mji Jirani wa Hanin. Pamoja na kutokuegemea upande wowote wa mzozo kati ya Israel na Hezbollah, jeshi hilo limekuwa likishambuliwa na hadi sasa wanajeshi wake kadhaa wameshauwawa.

Soma zaidi: Watu 87 wauawa au kupotea Kaskazini mwa Gaza

Kwingineko, Wizara ya afya ya Gaza imesema idadi ya watu waliouwawa au waliotoweka baada ya mashambuliuzi ya anga ya Israel huko Beit Lahiya imefikia watu 87. Kulingana na wizara hiyo iliyo chini ya kundi la Hamas, idadi hiyo ya vifo ni kubwa zaidi kuripotiwa ndani katika shambulio moja katika miezi kadhaa iliyopita.Israel kwa upande wake imesema inachunguza ripoti kuhusu tukio hilo.