Kundi la mwisho la kikosi cha Ufaransa kuondoka Niger leo
22 Desemba 2023Matangazo
Licha ya kuondoka kwa jeshi la Ufaransa, mamia ya wanajeshi wengine wa Marekani, Italia na Ujerumani bado wamesalia nchini humo.Ufaransa ilisema itawaondoa takriban wanajeshi wake 1,500 na marubani kutoka nchini Niger baada ya utawala mpya wa kijeshi kuwataka waondoke nchini humo kufuatia mapinduzi ya Julai 26.Hii ni mara ya tatukatika muda wa chini ya miezi 18 ambapo wanajeshi wa Ufaransa wametakiwa kuondoka katika taifa la ukanda wa Sahel.Jeshi hilo lililazimika kuondoka pia katika makoloni yake ya zamani ya Mali na Burkina Faso baada ya kutokea mapinduzi ya kijeshi kwenye mataifa hayo mawili.