1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Uingereza yafuja fedha za msaada kwa Malawi

28 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEgi

Serikali ya Uingereza imefuja maelfu ya paundi ya fedha za msaada zilizotegwa kwa ajili ya Malawi.

Repoti ya Radio ya Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC imesema kwamba paundi milioni tatu sawa na dola milioni tano nukta 42 zilizotolewa michango kwa miradi ya Malawi na Idara ya Msaada wa Maendeleo ya Uingereza DFID karibu paundi 600,000 zilitumika kwa mahoteli kwa ajili ya wataalamu wa ushauri wa Kimarekani katika kipindi cha zaidi ya miaka minne na fedha nyengine paundi 126,000 zilitumika kwa ajili ya chakula.

Msemaji wa DFID ametetea mipango ya idara yake lakini amekiri kwamba gharama za mradi mmoja unaohusisha wakala wa ushauri wa Marekani ambayo ni Taasisi ya Taifa ya Demokrasia zilikuwa kubwa mno.

Malawi ambayo haina bahari ni mojawapo ya nchi maskini kabisa duniani na wengi wa watu wake wanaofikia milioni 11 wanaishi kwa kutegemea pungufu ya dola moja kwa siku.