1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maaskofu wa Kikatoliki Afrika wapinga kuwabariki mashoga

29 Desemba 2023

Maaskofu wa Kikatoliki barani Afrika, wamepinga agizo la hivi karibuni la Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis la kuwabariki watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

https://p.dw.com/p/4aiZ6
Vatikan 2023 |  Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa FrancisPicha: Tiziana Fabi/AFP/Getty Images

Wakatoliki wa kihafidhina wamelaani tamko la Vatican ambalo liliidhinishwa na Papa Francis.

Maaskofu kutoka Kenya, Uganda, Angola, Nigeria, Malawi, Zimbabwe na Sao Tome na Principe, ni miongoni mwa makasisi ambao wamesema hawatabariki kamwe watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, kitendo ambacho ni kosa katika mataifa mengi ya Afrika.

Soma pia:Papa aridhia kubariki mahusiano ya jinsia moja yasiofanana na ndoa

Katika kanisa la Anglikana, suala hilo limesababisha mgawanyiko mkubwakwa zaidi ya miongo miwili, lakini hadi sasa Kanisa Katoliki limejaribu kuficha uwepo wa migogoro kutokana na suala hilo.