Maaskofu waonya kuhusu kucheleweshwa uchaguzi DRC
2 Machi 2021Uchaguzi mkuu unatarajiwa nchini humo mwishoni mwa mwaka 2023, mwaka ambao huenda ukapita bila chochote kufanyika kutokana na hali ya mashaka inayoendelea kushuhudiwa, na picha ya huzuni iliyotafsiriwa na maaskofu wa Kanisa Katoliki.
"Hakutakuwa na udhuru wa kutofanya uchaguzi mkuu uliopangwa hapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 2023 ujao," walitilia mkazo maaskofu hao katika ujumbe uliopewa kichwa: "Rarua moyo wako na sio nguo zako, watu bado wanasubiri".
Kwa mjibu wa maaskofu hao, kuna pengo kubwa kati ya ahadi kutoka mamlaka na ukweli hapa nyumbani, na wananchi wanaishi katika hali isiyo na uhakika.
Soma pia: Kinshasa: Waandamanaji wawili wauawa kwa kupigwa risasi
"Serikali ifanye marekebisho ya uchaguzi kuwa moja ya vipaumbele, ili kuboresha usimamizi wa uchaguzi na kuimarisha demokrasia," alisema padri Donatien Tshole, katibumkuu wa CENCO.
Ameitaka serikali kufanya kila liwezekanalo ili kuandaa uchaguzi wa kuaminika, ulio wazi, na wa amani mnamo mwaka 2023 na sio baadaye.
Tume ya uchaguzi yaungana na Maaskofu
Kwa upande wake, kiongozi wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) Corneille Nangaa ametoa mwito kwa serikali kuwa tayari kuandaa uchaguzi huo wa 2023, na kusema kwamba hilo ndiyo litaepusha kucheleweshwa uchaguzi kama ilivyotokea 2016.
Soma pia: Asasi za kiraia zalia na hitilafu uchaguzi DRC
"Nawaomba viongozi wasisubiri kuzindua maandalizi ya uchaguzi huu, pamoja na kuwekwa kwa viongozi wapya watakaochukua nafasi yetu. Kuanzisha mageuzi ya kweli ambayo hayatapingana na utayarishaji wa uchaguzi ujao."
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inapaswa kuandaa kwa wakati mmoja, uchaguzi wa rais, wabunge, manispaa na mitaa.