Macron aanza ziara ya kimkakati katika eneo la Asia ya Kati
1 Novemba 2023Macron anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenzake Kassym-Jomart Tokayev, pamoja na kusaini mikataba ya ushirikiano katika sekta anga na utengezaji wa dawa.
Mwaka jana, mahusiano ya kibiashara kati ya Ufaransa na Kazakhstan yalifikia dola bilioni 5.6 huku Astana ikiipatia Paris karibu asilimia 40 ya mahitaji yake ya Urani. Ziara ya Macron huko Kazakhstan ni ya kwanza kwa rais wa Ufaransa tangu mwaka 1994.
Macron atalitembelea pia taifa la Uzbekistan katika eneo la Asia ya Kati ambako Urusi, China, Uturuki na mataifa ya Ulaya wamekuwa wakigombea ushawishi kutokana na utajiri wake wa nishati. Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wanatarajiwa pia kuzuru Astana siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii.