Wengi wataka choloroquine itumike kutibu corona Ufaransa
6 Aprili 2020Matangazo
Jambo hili limezua mjadala mkubwa miongoni mwa wataalamu wa afya kote ulimwenguni. Uungaji mkono wa dawa hiyo kwa matibabu ni jambo ambalo wengi wanataka lifanyike wakati ambapo madaktari wanajaribu wasipokee wagonjwa zaidi wa covid-19 wasifike katika hospitali ambazo zimelemewa na mzigo wa wagonjwa.
Wengine wanasema hilo ni jambo zuri ambalo huenda likamfanya mgonjwa asifikie hatua ya kufikishwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Rufaa hiyo iko katika tovuti ya Change.org na ilianzishwa Ijumaa na kundi moja la madaktari na waziri wa zamani wa afya wa Ufaransa.
Waziri wa afya wa Ufaransa Olivier Veran alitaka kuwepo na tahadhari katika matumizi ya dawa hiyo akisema matokeo ya awali kuhusiana na matumizi yake yatatolewa hivi karibuni.