1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya watu wahamishwa Italia kufuatia Kimbunga Boris

19 Septemba 2024

Mamlaka nchini Italia imewahamisha takriban watu 1,000 baada ya kimbunga Boris kupiga hapo jana kwenye eneo la kaskazini mashariki la Emilia-Romagna na Marche na kusababisha mafuriko makubwa.

https://p.dw.com/p/4krYA
Mafuriko Italia
Wakazi wanahamishwa na wafanyikazi wa dharura baada ya mto Nysa Klodzka kufurika mji wa Lewin Brzeski kusini magharibi mwa Poland, Septemba 17, 2024.Picha: Beata Zawrzel/Zuma/IMAGO

Naibu Waziri wa Uchukuzi Galeazzo Bignami amewaambia waandishi wa habari kwamba watu wawili haijulikani walipo. Shule zilifungwa na huduma za treni zimesitishwa kwa muda. Upepo mkali na mvua kubwa vimeshuhudiwa Ulaya ya kati na mashariki na kuua takriban watu 24. Kimbunga Boris kimasababisha mafuriko na kuyaathiri mataifa ya Austria, Jamhuri ya Czech, Poland na Romania. Wataalamu wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na utoaji wa gesi chafuzi inayotokana na shughuli za binadamu, yanaongeza kasi ya majanga hayo ya asili.