1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yaua 14 Bosnia Herzegovina

4 Oktoba 2024

Watu wasiopungua 14 wamekufa kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba Bosnia Herzegovina na mkoa wa milimani wa Herzegovina-Neretva ulio kusini mwa nchi hiyo ndiyo umeathiriwa zaidi na janga hilo.

https://p.dw.com/p/4lQKp
Mafuriko Ulaya
Mafuriko makubwa yameuwa watu 11 nchini Bosnia-HerzegovinaPicha: RUSMIR SMAJILHODZIC/AFP

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mvua kubwa iliyonyesha imesababisha kingo za mito kadhaa kupasuka huku mji wa Jablanic umekumbwa na maporomoko ya udongo yaliyosomba nyumba nyingi.

Mawasiliano na mji huo yamekatika baada maji kuharibu barabara na kusomba njia ya reli. Waokoaji wamefanikiwa kuufikia mji huo kwa kutumia boti na ripoti zinasema watu wengine wameokoloewa. 

Soma zaidi: EU yatenga euro bilioni 10 kwa nchi zilizoathiriwa na mafuriko

Msemaji wa serikali ya mkoa wa Herzegovina-Neretva amewambia waandishi habari kwamba kwa kumbukumbu alizonano hilo ndiyo janga kubwa zaidi kuikumba Bosnia Herzegovina tangu kumalizika kwa vita vya kanda ya Balkani vya mwaka 1992 hadi 1995.