Mali yamfukuza balozi wa Sweden
10 Agosti 2024Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Mali ilitangaza hapo jana kwamba balozi huyo amepewa masaa 72 kuondoka, baada ya Waziri wa Misaada ya Maendeleo na Biashara ya Nje wa Sweden, Johan Forssell, "kutoa matamshi mabaya dhidi ya Mali".
Tayari, Sweden ilikuwa imeshatangaza tangu mwezi Juni kwamba ingeliufunga ubalozi wake mjini Bamako na pia kwenye nchi jirani, Burkina Faso, kufikia mwishoni mwa mwaka huu, na kusitisha misaada kwa mataifa hayo na mengine kadhaa.
Soma zaidi: Ukraine yasikitishwa na kuvunjika uhusiano na Niger
Jumatano iliyopita, Forssell aliandika kwenye mtandao wa X kwamba wanaounga mkono vita vya Urusi nchini Ukraine, wasitarajie kupokea fedha za misaada kutoka Sweden.
Mali imekuwa ikipata msaada wa kijeshi kupitia mamluki wa Kirusi tangu mwaka 2021 na hivi karibuni ilivunja uhusiano wake na Ukraine.