SiasaMarekani
Marekani, Japan na India zatangaza mikakati ya kiusalama
29 Julai 2024Matangazo
Wanadiplomasia hao wamejadili pia njia za kusimamia usalama wa kimtandao na kuzisaidia nchi nyingine za Asia na Pasifiki katika kuimarisha mifumo yao ya ulinzi.
Hatua hiyo inachukuliwa kufuatia kuongezeka kwa mivutano katika maeneo ya bahari ya kanda hiyo.
Soma pia: NATO yalenga kukabiliana na ushawishi wa China
Mawaziri wa mambo ya nje wa Japan, Marekani Australia na India wamesema wana wasiwasi mkubwa kuhusu mivutano iliyopo na wamekosoa vikali hatua zinazochukuliwa na China katika eneo la bahari ya Kusini mwa China.
Serikali nyingi za kanda hiyo zinapingana na madai ya China kuhusu kumiliki eneo bahari ya Kusini mwa China ambalo ni eneo muhimu kwa shughuli za kibiashara na kuna uwezekano wa kuwepo nishati katika eneo hilo.