1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaiomba China kuitaka Iran iwazuwie Wahouthi

24 Januari 2024

Marekani imeiomba China izungumze na Iran juu ya kuitaka nchi hiyo iwadhibiti waasi wa Houthi wanaofanya mashambulizi ya kuzilenga meli za mizigo katika Bahari ya Sham.

https://p.dw.com/p/4bcLN
Waziri wa Nje wa Nje wa Marekai Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken, anaitaka China izungumze na Iran juu ya kuwazuwia Wahouthi wasishambulie meli kwenye Bahari ya Sham.Picha: Ângelo Semedo/DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amelizungumzia suala hilo na mwenzake wa China, akiongeza kuwa Marekani inaamini China haijaweka shinikizo lolote kwa Iran juu ya kuwadhibiti Wahouthi waanaofanya mashambulizi, licha ya kauli ya Beijing ya wiki iliyopita ambayo haikuwa na uzito.

Mapema siku ya Jumatano (Januari 24), majeshi ya Marekani na Uingereza yalishambulia na kuharibu meli mbili za Wahouthi ambazo mataifa hayo yanadai zilikuwa zinajiandaa kufyatua makombora kuelekea kwenye Bahari ya Sham.