Marekani yasema mazungumzo na china ni muhimu kuepuka Mzozo
3 Juni 2023Matangazo
Licha ya wawili hao kupeana mkono na kuzungumza kwa ufupi, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kilele wa masuala ya usalama unaofahamika kama jukwaa la Shangri-La nchini Singapore, mawasiliano kati yao yalishindwa kutoa matumaini kwa Marekani ya uwepo wa mazungumzo kati yao.
Austin anaamini mazungumzo kati yao ni muhimu hasa kati ya viongozi wa ulinzi na wale wa kijeshi, lakini China imesema Marekani inajua ni kwanini kuna ugumu wa viogozi hao kukutana.
Kanali Zhao Xiaozhuo alisema China pia inaamini mazungumzo kati yao yanahitajika lakini ni lazima kwanza Marekani iache kuyumbisha usalama wa China.