1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema Urusi iliidugua kimakosa ndege ya Azerbaijan

28 Desemba 2024

Taarifa za intelijensia ya Marekani zinasema kuwa Urusi huenda iliiangusha kimakosa ndege ya abiria ya Azerbaijan, ikiidhania kuwa droni ya mashambulizi.

https://p.dw.com/p/4odcG
Kazakhstab | Aktau Ajali ya ndege ya Azebaijan
Watu 38 waliuawa na wengine 29 walijeruhiwa kwenye ajali ya ndege ya Azerbaijan.Picha: inistry of Emergency Situations of Kazakhstan/Anadolu/picture alliance

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la MSNBC ikinukuu vyanzo viwili vya jeshi la Marekani. Ndege hiyo ilianguka Kazakhstan Jumatano, na dalili za awali zinaonyesha ililengwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi.

Waziri wa Azerbaijan, Rashan Nabiyev, alirejelea ushahidi wa wataalamu na maelezo ya manusura kuthibitisha madai hayo.

Soma pia: Wataalamu wa anga wasema mifumo ya Urusi huenda iliiangusha ndege ya Azerbaijan

Taarifa za wataalamu wa anga zinaeleza kuwa mifumo ya Urusi ilijibu shambulio la Ukraine, na kuongeza shinikizo kwa Urusi, ambayo inadai kulikuwa na shambulio la droni karibu na eneo ambako ndege hiyo ilikuwa ikielekea kutua.

Msemaji wa Baraza la Usalama la White House, John Kirby, alithibitisha uwepo wa ushahidi wa awali lakini akakataa kutoa maelezo zaidi kutokana na uchunguzi unaoendelea.