Marekani yaonya kuhusu uwezekano wa mashoga kushambuliwa
18 Mei 2024Matangazo
Taarifa hii inawataka Wamarekani kuchukua tahadhari wanaposafiri bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi au kutaja vitisho vinavyoongezeka dhidi ya jamii ya LGBTQ. Hivi karibuni, baadhi ya nchi zimepitisha sheria kali dhidi ya mashoga.
Soma pia: Biden akosoa sheria ya Uganda dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuhimiza kufutwa
Mwezi uliopita, Bunge la Iraq liliidhinisha sheria ambayo inatoa adhabu kali kwa mashoga na watu waliobadili jinsia huku Mahakama ya Uganda nayo ikipitisha sheria inayotoa hukumu ya kifo kwa vitendo vinavyotajwa kuwa "ushoga uliokithiri."