1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yauwa mtu 1 Lebanon

9 Desemba 2024

Lebanon limesema mtu mmoja ameuawa hii leo Jumatatu katika mashambuzi ya Israel katika eneo la kusini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4nurE
Libanon Dahiyeh | Flammen und Rauch nach einem israelischen Luftangriff
Picha: Bilal Hussein/AP Photo/picture alliance

Katika mashambulizi hayo, wanajeshi wanne wa Lebanon wamejeruhiwa huku makubaliano ya kusitisha vita ambayo ni hafifu yakiendelea kutekelezwa.

Jeshi la Israel katika taarifa yake limesema mashambulizi hayo yalitokea pale maadui walipolilenga gari moja karibu na kizuizi cha kijeshi cha Saf al-Hawa/Bint Jbeil.

Waziri wa Afya wa Lebanon, Firass Abiad, amesema mpaka sasa idadi ya watu waliouawa katika vita vya zaidi ya mwaka mmoja kati ya Israel na Hezbollah imefikia watu 4,047 wakiwemo watoto 316.