1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya Olimpiki katika mto Seine yaahirishwa

Josephat Charo
30 Julai 2024

Viwango visivyo salama vya usafi katika mto Seine vimelazimu mashindano ya wanaume ya triathlon kwenye michezo ya Olimpiki yaahirishwe hivi leo.

https://p.dw.com/p/4iu6D
Ufaransa Paris 2024 | Watalii huchukua picha ya nembo ya Olimpiki kwenye Bastille
Watalii wakipiga picha ya nembo ya Olimpiki huko Bastille - Julai 25, 2024 Paris Ufaransa,Picha: Bernd Kammerer/Presse- und Wirtschaftsdienst/picture alliance

Katika pigo kubwa kwa mashindano hayo, waandaaji wa Olimpiki wamekuwa wakisisitiza mara kwa mara kwamba mto huo ungekuwa salama kwa kuogelea, lakini mashindano ya michezo mitatu ya kuogelea yaliyokuwa yafanyike leo yamefutwa saa chache kabla kuanza, kufuatia matokeo ya mwisho ya ubora wa maji. Taarifa ya pamoja ya waandaaji wa Olimpiki Paris 2024 na kamati ya kimataifa ya michezo ya Triathlon imelaumu ongezeko la viwango vya uchafuzi kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris Ijumaa na Jumamosi iliyopita. Mashindano ya wanaume katika mto huo yamepangwa kufanyika kesho Jumatano, lakini uwezekano wa mvua kubwa kunyesha tena leo mjini Paris unaibua maswali ikiwa kweli mashindano hayo yatafanyika kama yalivyoahirishwa.