1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Antony Blinken akutana na Subrahmanyam Jaishankar

11 Novemba 2023

Mawaziri wa mambo ya kigeni na wale wa ulinzi wa India na Marekani wamekutana mjini New Delhi leo kwa ajili ya mazungumzo yatakayoboresha ushirikiano baina yao sambamba na kutathimini changamoto za kikanda zinazoendelea

https://p.dw.com/p/4Yg98
Viongozi wa Marekani Antony Blinken na Lloyd Austin pamoja na viongozi wa India  Subrahmanyam Jaishankar na Rajnath Singh katika picha ya pamoja.
Viongozi wa Marekani Antony Blinken na Lloyd Austin pamoja na viongozi wa India Subrahmanyam Jaishankar na Rajnath Singh katika picha ya pamoja.Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Ulinzi Lyold Austin wamekutana na wenzao wa mambo ya nchi za nje wa India Subrahmanyam Jaishankar na yule wa ulinzi  Rajnath Singh kwa mazungumzo ya kila mwaka yanayofahamika kama 2+2 yanaowaleta pamoja mawaziri wa sekta hizo mbili. 

Wamesema ajenda ya majadiliano ilikuwa ni kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuleta ushirikiano wa ulinzi na usalama, lakini pia wamejadili kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya India na China, uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na changamoto zilizochochewa na mzozo wa Gaza.

Soma zaidi: Blinken afanya mazungumzo ya faragha na mwenzake wa Uturuki

Wakati wa mkutano huo Blinken amesema ''tuna mengi ya kufanya pamoja ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na wenzetu na hilo tunasubiri sana . Na nadhani ni ushahidi zaidi wa mtazamo wetu thabiti kutoka Marekani juu ya kanda ya Bahari ya Hindi na Pasifiki , eneo la kimkakati kwa siku zijazo, na wakati wenyewe kwa hakika ni sasa na tunajenga msingi huo wa hilo pamoja na India. Kwa hivyo nina matumaini makubwa na mazungumzo haya. 

Kwa upande wake Llyod Austinamesema ''Wakati huu wa changamoto za dharura za kimataifa, ni muhimu zaidi sasa kwa mataifa mawili makubwa dunian kubadilishana maoni, kufikia malengo sawa na kwajibikia raia wetu. Tumepata mafanikio ya kuvutia katika kujenga ushirikiano wetu mkuu wa ulinzi katika mwaka uliopita na hiyo itatusaidia kuchangia kuleta amani na utulivu''

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa mambo ya nje wa India Subrahmanyam Jaishankar wakapeana mkono.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa mambo ya nje wa India Subrahmanyam Jaishankar wakipeana mkono.Picha: Jonathan Ernst/REUTERS

Katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, uhusiano wa Marekani na India umeendelea kuwa madhubuti katika maeneo mbalimbali, ingawa serikali ya India vilevile imeendelea kuwa na uangalifu katika kuulinda uhusiano uhusiano wake wa muda mrefu na Urusi, na hasa kutokana na m ahusano mabaya na mataifa ya magharibi yaligubikwa na vita vya Ukraine.

India na Marekani zimetangaza kuingia mikataba ya ushirikiano juu ya masuala ya ulinzi na usalama ili kukabiliana na changamoto za kijiografia na kisiasa kama nchi wanachama na wanadiplomasia. 

Nchi hizo mbili ambazo mara moja ziliwahi kutofautiana kwa sasa watafanya kazi kwa mikataba iliyotajwa kuwa ya kihistoria ikiwa ni pamoja na Marekani kuwa msambazaji na mtengenezaji wa injini za ndege za kivita zaIndia.