1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mawaziri wa Korea Kusini, Japan na China kukutana Jumapili

24 Novemba 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini, Japan na China watafanya mazungumzo yao ya kwanza ya pande tatu mwishoni mwa jumaa huko Busan nchini Korea Kusini ikiwa ni ya kwanza tangu 2019.

https://p.dw.com/p/4ZObK
Waziri wa Mambo ya Nje Japan Fumio Kishida pamoja na Rais wa China Xi Jinping
Waziri wa Mambo ya Nje Japan Fumio Kishida pamoja na Rais wa China Xi JinpingPicha: Kyodo News via AP/picture alliance

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa leo na wizara ya mambo ya nje ya Seoul.

Mkutano huo wa siku ya Jumapili kwenye mji huo wa mwambao, utawakutanisha Park Jin, Yoko Kamikawa na Wang Yi wanaotarajiwa kujadili kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya ushirikiano wa pande tatu, hali jumla ya kikanda na kimataifa.

Soma pia:China na Japan zathibitisha uhusiano wa kimkakati

Hayo yanaarifiwa siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanikiwa kurusha satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi, jambo lililopelekea kusitishwa kwa makubaliano ya kijeshi yaliyodumu kwa miaka mitano kati ya Seoul na Pyongyang yaliyonuiwa kupunguza mvutano kwenye rasi ya Korea.