1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa nishati wa G7 kujadili miundombinu ya Ukraine

20 Septemba 2024

Mawaziri wa nishati wa kundi la nchi saba zilizoinukia zaidi kiviwanda (G7) watakutana siku ya Jumatatu ili kujadili hali ya miundombinu ya nishati ya umeme ya Ukraine iliyoharibiwa vibaya na vita.

https://p.dw.com/p/4kuX9
Moshi ukizuka baada ya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine.
Moshi ukizuka baada ya mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine.Picha: SERGEI SUPINSKY/AFP via Getty Images

Tangu uvamizi kamili wa Moscow mnamo Februari 2022, mifumo ya nishati ya Ukraine imekuwa ikilengwa na mashambulizi ya Urusi na kusababisha matatizo ya ugavi wa umeme.

Soma zaidi: Scholz: Mapendekezo ya Putin kuhusu Ukraine hayana uhalisia

Hayo yakiarifiwa, Umoja wa Ulaya umesema unalenga kuikopesha Ukraine kiasi cha dola bilioni 39 kutoka kwa mapato ya mali za Urusi yaliyozuiwa katika umoja huo.

Norway, kwa upande wake, imesema itaongeza msaada wa kiraia kwa Ukraine dola milioni 475 na kutanua mpango wake wa msaada kwa miaka mitatu hadi 2030.