1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchezaji wa Slovakia aambukizwa Corona

17 Juni 2021

Mlinzi wa Slovakia Denis Vavro na mmoja wa wanachama wa benchi la ukufunzi wa timu hiyo wamethibitishwa kuambukizwa Covid-19 kabla ya mechi ya dhidi ya Sweden.

https://p.dw.com/p/3v73c
EURO 2020 Fußball Qualifikation Mannschaft Slowakei
Picha: Mike Griffiths/imago images

Kocha wa Slovakia Stefan Tarkovic ametoa taarifa ya maambukizo ya wawili hao, hiki kikiwa kisa cha kwanza kutangazwa tangu kuanza kwa michuano ya kuwania kombe la EURO 2020. soma  Mostovoy wa Urusi nje ya kikosi

Tarcovic amesema Vavro hana dalili zozote na sasa amejitenga, lakini hakutaja jina la kocha aliyeambukizwa.

Upimaji ulifanyika katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo huko St. Petersburg jana Jumatano, siku mbili baada ya mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Poland iliyochezwa mji mkuu wa Urusi. soma Euro 2020: Italia yaitandika Uturuki bao 3-0

Slovakia inatarajiwa kushuka dimbani kuchuana na Sweden siku ya Ijumaa huko St.Petersburg.

Itifaki za UEFA

Russland St. Petersburg | UEFA Euro 2020 | Polen v Slowakei
UEFA Euro 2020Picha: Anton Vaganov/AP/picture alliance

"Tulianza kufanya kazi na mamlaka ya afya ya umma ya Urusi na kuanza kutumia itifaki zinazotakiwa na UEFA. Kwa hivyo tulichukua hatua zote ili kuepuka kuenea kwa maambukizo." alisema Tarkovic kupitia mkalimani.

Itifaki za shirikisho la soka Barani Ulaya UEFA zinasema kwamba timu zilizo na wachezaji chini ya 13 mchezo wao unaweza "ukaahirishwa ndani ya masaa 48 ya tarehe ya mechi iliyopaswa kuchezwa ” na kuna uwezekano wa kubadilishwa kwa kiwanja tofauti.

Shirikisho la UEFA limeongeza kuwa "Mchezaji yeyote wa ziada akiitwa ili kufikia kiwango cha chini cha wachezaji 13 inahitaji kwamba idadi sawa ya wachezaji waliotengwa wanaondolewa kabisa kutoka kwa orodha ya wachezaji 26. "

Kulusevski arudi dimbani

Russland St. Petersburg | UEFA Euro 2020 | Tor Slowakei
Picha: Kirill Kudryavtsev/REUTERS

Wachezaji wa Sweden Dejan Kulusevski na Mattias Svanberg walipatikana na Corona kabla ya kuanza kwa mashindano ya EURO 2020. Kulusevski anatarajiwa kushiriki katika mechi inayokuja dhidi ya Slovakia katika Uwanja wa Saint Petersburg.

Siku ya Ijumaa saa chache kabla ya mechi ya kwanza ya michuano ya EURO 2020, kati ya  Italia na Uturuki, Urusi ilitangaza kwamba winga Andrey Mostovoy alithibitishwa kupata maambukizi ya Covid-19.

Katika itifaki zake, UEFA inasema ikiwa kuna waliothibitishwa kuambukizwa timu "lazima zitekeleze mpango mkali wa kutafuta waliowasiliana nao kwa ajili ya orodha ya upimaji."

Mamlaka ya St Petersburg wiki hii imeimarisha vizuizi katika juhudi za kuzuia maambukizo. Pamoja na kufunga maeneo ya kula katika maduka makubwa ya jiji na eneo la mashabiki wa Euro 2020. soma Timu ya Ujerumani yashindwa kutamba mbele ya Ufaransa

Slovakia iliifunga Poland mabao 2-1 katika mchezo wake wa kwanza katika Kundi E. Vavro mwenye umri wa miaka 25 alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika katika mechi hiyo.

"Ni hali ngumu kwa mchezaji, ambaye ana kazi kubwa mbele yake na alikuwa na matarajio makubwa katika michuano hii ya Euro, hivyo ni aibu kuwa yuko nje kwa sababu ya hali hiyo." Tarkovic alisema.

 

/APE