Mechi za kufuzu CHAN 2025 zaendelea barani Afrika
23 Desemba 2024Michuano ya kandanda ya kufuzu kwa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN)ambayo inawahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani barani humo imeendelea katika viwanja mbalimbali usiku wa kuamkia leo.
Nigeria imetoka sare ya 0-0 dhidi ya majirani zao Ghana. Wakati huo huo, mabingwa watetezi Senegal walichukua uongozi ambao ulidumu kwa dakika sita pekee katika sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Liberia mjini Paynesville.
Soma zaidi.Ghana huenda ikashindwa kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa Afrika
Katika mchezo mwingine Ivory Coast walipata uongozi wa 2-0 dhidi ya Burkina Faso mjini Abidjan huku Sudan ikiivurumisha Ethiopia kwa magoli 2-0.
Michuano hiyo itafanyika mapema mwakani ambapo nchi za Tanzania,Kenya na Uganda zinayaandaa mashindano hayo kwa pamoja.