1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea binafsi Namibia apinga matokeo ya uchaguzi

19 Desemba 2019

Aliyekuwa mgombea binafsi wa urais wa Namibia Panduleni Itula, amewasilisha pingamizi la kisheria ya kupinga kushindwa kwake katika uchaguzi uliomalizika mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/3V6Ll
Namibia Wahlen
Picha: picture-alliance/dpa/S. Smith

Itula ameitaka mahakama ya juu ya Namibia kuagiza kurejewa uchaguzi haraka iwezekenavyo, kwa madai kwamba haukuwa huru. Katika faili lake la kurasa 126, mgombea huyo amebainisha makosa yaliyojitokeza kutokana na matumizi ya mashine za kielektroniki kwenye uchaguzi.

Hata hivyo mahakama ya juu bado haijapanga tarehe ya kusikiliza madai yake. Rais Hage Geingob wa chama tawala cha SWAPO, anatarajiwa kuapishwa kwa muhula mpya mnamo Machi 21 baada ya kushinda tena uchaguzi wa muhula wa pili wa miaka mitano.

Uungwaji mkono wake umeshuka kutoka asilimia 87 aliyoipata 2014 hadi asilimia 56 huku kukiwa na hasira ya umma juu ya kashfa za ufisadi na ukosefu wa ajira.