Mgombea urais Tunisia ahukumiwa miaka 12 jela
1 Oktoba 2024Matangazo
Wakili wa Ayachi Zammel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba bado mwanasiasa huyo anabakia kuwa mgombea katika uchaguzi huo wa rais unaofanyika siku ya Jumapili (Oktoba 6).
Soma zaidi: Makumi ya wanachama wa Ennahda wakamatwa kuelekea uchaguzi Tunisia
Zammel ambaye ni mbunge wa zamani na mfanyabiashara anaongoza chama kidogo cha kiliberali na amekuwa ni mmoja kati ya wagombea wawili walioidhinishwa na Tume ya Uchaguzi ya Tunisia kupambana na Rais Kais Saed katika uchaguzi huo wa rais.
Tume ya uchaguzi imewazuia kiasi cha wagombea wengine 14 kuwania kwenye uchaguzi huo.