Michelle Bachelet ana wasiwasi juu ya hali ya Kashmir
9 Septemba 2019Mkuu huyo wa shirika la kutetea haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, amesema ana wasiwasi juu ya athari ya hatua ya serikali ya India na masuala ya haki za binaadamu ya watu wa Kashmir.
Akizungumza katika Baraza la Haki za binaadamu la Umoja huo Bachelet amesema kukatiwa kwa mawasiliano ya intaneti, maandamano ya amani na kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa na wanaharakati ni mambo yanayompa wasiwasi.
"Ofisi yangu inaendelea kupata ripoti ya hali ya haki za binaadamu kwa pande zote mbili. Huku nikiendelea kuitolea mwito serikali ya India na Pakistan kuhakikisha haki zabinaadamu zinaheshimiwa na kulindwa, nimeiomba hasa India kuondoa hali ya dharura kuhakikisha watu wanafikia huduma muhimu," alisema Bachelet.
India ilitangaza hali ya dharura Kashmir tangu Agosti 5 kuzuwia machafuko wakati ilipoiondolewa hadhi yake eneo hillo linalozozajiwa huku mawasiliano ya simu ya mkononi na mawasiliano ya intaneti ikiwa hadi sasa imekatwa.
Jimbo la Kashmir ni chanzo cha uhasimu kati ya India na Pakistan
Jimbo la Kashmir, lililogawika kati ya India na Pakistan tangu mwaka 1947, limekuwa chanzo cha mvutano kati ya mataifa hayo mawili yanyomiliki silaha za nyuklia na kusababisha mapigano ya mara kwa mara.
Hata hivyo Bachelet amesema ni muhimu kwa watu wa Kashmirkushauriwa katika maamuzi ya aina yoyote yatakayokuwa na athari ya siku za usoni kwa jimbo hilo. Tamko lake linakuja baada ya serikali ya India siku ya Jumapili kuimarisha usala katika jimbi hilo baada ya kutawanya maandamano ya kidini yaliyofanywa na waislamu wa kishia waliokiuka marufuku ya kuandamana.
Bachelet pia ameelezea wasiwasi wake juu ya suala tata la usajili wa uraia katika jimbo la Assam ambao wakosoaji wanahofia ni mpango wa chama tawala cha Hindu-nationalist Bharatiya Janata kuwaondoa waislamu.
Takriban watu milioni 1.9 wameondolewa katika orodha ya kupata uraia iliyochapsihwa Agosti 31 hali iliyoleta hofu na kuchanganyikiwa miongoni mwa wakaazi wa eneo hilo. Ametaka serikali kuzuwia kuwakamata na kuwafukuza watu kwa lazima na kuhakikishwa wanalindwa kutokuwa wakosa dola.
Hata hivyo waziri wa mambo ya kigeni wa Pakistan Shah Mehmood Qureshi anatarajiwa kulihutubia baraza la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa haüpo kesho Jumanne kwa hotuba inayotarajiwa kugusia kwa kiwango kikubwa mzozo huo wa Kashmir
Chanzo: afp