Misikiti tisa mashuhuri Afrika
Bara la Afrika linajivunia kuwa na misikiti ya kuvutia. Picha zifuatazo zinaonyesha misikiti inayoakisi karibu kila kipindi cha usanifu wa ujenzi katika historia. Kutoka 670 Baada ya Kristo hadi 2019.
Msikiti wa Massalikul Jinaan, Senegal
Msikiti wa Massalikul Jinaan ulimalizika Septemba 2019 kwa gharama ya euro milioni 30 na watu wa madhehebu ya Udugu wa Murid. Ni msikiti mkubwa zaidi Afrika Magharibi. Watu zaidi ya 15,000 wanaweza kusali ndani yake, na nje kuna uwanja wenye nafasi ya kutosha ya kusali watu wengine 15,000. Jina la msikiti huo limetokana na shairi la Sheikh Ahmadou Bamba Mbacke, mwanzilishi wa Udugu wa Murid.
Msikiti Mkubwa wa Kairouan, Tunisia
Msikiti huu mzuri ni moja wapo ya sehemu za zamani za ibada katika ulimwengu wa Kiislam, na pengine ni msikiti wa zamani zaidi barani Afrika. Umejengwa mnamo mwaka 670 na jenerali wa Kiarabu Uqba ibn Nafi. Msikiti huu unaonyesha mchanganyiko wa usanifu wa ujenzi wa kabla ya Uisilamu, Ufalme wa Kirumi na utawala wa Byzantine.
Msikiti wa Larabanga, Ghana
Maarufu unajulikana kama msikiti wa Makka wa Afrika Magharibi, msikiti wa Larabanga umejengwa mwaka 1421kwa usanifu wa ujenzi wa watu wa Sudan katika kijiji cha Larabanga, Ghana. Ni msikiti wa zamani zaidi nchini humo na pia katika eneo zima la Afrika Magharibi. Umeorodheshwa miongoni mwa majengo yanayoweza kupotea duniani, na umeshafanyiwa ukarabati mara kadhaa.
Msikiti wa Touba, Senegal
Msikiti mkubwa wa Touba ulianza kujengwa mwaka 1887 na muumini wa madhehebu ya Sufi na mwanzilishi wa Udugu wa Murid, Amadou bamba - hata hivyo haukumalizika kujengwa hadi 1963. Bamba alifariki dunia 1927 na alizikwa nje ya msikiti huo ambao sasa unasimamiwa na vizazi vyake. Unatambuliwa kama moja wapo ya misikiti mizuri na inayopendeza duniani.
Msikiti Mkuu wa Djenne, Mali
Msikiti Mkuu wa Djenne ni msikiti mkubwa zaidi duniani uliojengwa kwa matofali ya udongo. Ilijengwa mnamo 1907 kwa kutumia mtindo wa kipekee wa usanifu wa ujenzi ambao chimbuko lake ni karne ya 14 kutoka Sahel Magharibi.
Msikiti wa Kitaifa Abuja, Nigeria
Msikiti huu ulijengwa 1984 na unatambulika kama msikiti wa kitaifa Nigeria. Ingawa ulijengwa kwa ajili ya Wanaijeria Waislamu ambao idadi yako ni kubwa, lakini hata wasio Waislamu wanaruhusiwa kuingia, isipokuwa nyakati za swala. Umejengwa mkabala na Kituo cha kitaifa cha Kikristo.
Msikiti wa Kitaifa wa Uganda
Ulikamilishwa 2006, Msikiti wa Kitaifa wa Uganda ulioko jijini Kampala ni mfano wa usanifu wa kisasa wa misikiti. Ulifadhiliwa na kiongozi wa zamani wa Libyan , Muammar Gaddafi na kupewa jina lake. Baada ya kifo chake, jina hilo lilibadilishwa na pia unatumika kama makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu la Uganda.
Msikiti wa Hassan II, Morocco
Ujenzi ulikamilika 1993. Hadi hivi karibuni, Msikiti wa Hassan II ulikuwa ndiyo mkubwa zaidi barani Afrika na wa tatu dunuani. Ulijengwa kuadhimisha miaka 60 tangu kuzaliwa kwa alijekuwa Mfalme Hassan II. Umejengwa katika sehemu nzuri ya kilima kinachoikabili bahari. Eneo hilo limechaguliwa kusudi kutokana ana aya moja ya Qur-an inayosema, "kiti cha enzi cha Mungu kilijengwa juu ya maji."
Djamaa el Djazair, Algiers
Msikiti huu unajulikana pia kama Msikiti Mkuu wa Algiers, na ulijengwa kwa miaak saba na kugharimu zaidi ya dola bilioni 1. Ujenzi wake ulichangiwa duniani kote: fedha zilitolewa na serikali ya Algeria, wasanifu walitoka Ujerumani, na kujengwa na Shirika la Uhandisi la Serikali ya China.