1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misuko suko yamkumba Rais wa Malawi -Mutharika.

Saumu Mwasimba15 Julai 2005

Mwaka mmoja katika wadhifa wake rais Bingu wa Mutharika wa Malawi anakabiliwa na vitisho vya mashetani ,umasikini na uwezekano wa kung’olewa kutoka madarakani. Imeripotiwa kwamba mashetani wanamfuata rais huyo akiwa katika jumba lake la kifahari kwenye ikulu ya mjini Lilongwe. Lakini hata hivyo rais Bingu amekanusha madai hayo licha ya washauri wake wa kidini kutoa taarifa tofauti. Mwaka mmoja katika wadhifa wake rais Bingu wa Mutharika wa Malawi anakabiliwa na vitisho vya mashetani ,umasikini na uwezekano wa kung’olewa kutoka madarakani. Rais Bingu wa Mutharika ambaye alichukua madaraka baada ya kufanyika uchaguzi uliokumbwa na utata mnamo mwaka jana hivi sasa yu

https://p.dw.com/p/CHfs

po katika hali ya wasiwasi kufuatia vitisho kadha wa kadha. Mizuka inayojitokeza katika umbo la rais wa zamani wa nchi hiyo Bakili Muluzi inadaiwa kumfuata rais Bingu na hivyo kutatiza shughuli zake za kisiasa pamoja na kuzihujumu juhudi zake za kulijenga upya taifa hilo. Mfuasi wa Rais Bingu Agrippa Tembo akiulizwa kuelezea juu mafanikio ya kiongozi huyo katika kipindi hicho cha mwaka mmoja alicheka kwanza kisha akasema … Hadi kufikia sasa hakuna ufadhili wowote wa kifedha uliopatikana kusaidia bajeti ya nchi.pamoja na hayo Malawi ni mojawapo kati ya nchi za Afrika zilizokosa nafuu ya kupunguziwa madeni,hakuna mvua angalau ya kuwezesha ukulima wa vyakula huku maradhi ya ukimwi nayo yakichukua nafasi yake nchini humo. Alipoingia madarakani rais Bingu wa Mutharika kwanza alionekana kuwa kama kibaraka cha Muluzi, na bila kupoteza muda rais huyo alianzisha kampeini kabambe ya kupambana na rushwa akimlenga Muluzi pamoja na maswahiba zake. Akiandamwa na vitisho vya kungolewa madarakani kutokana na kuanzisha kamepini dhidi ya rushwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika chama cha UDF alichokuwa mwasisi mwenzi mnamo mwaka 1991,Wa Mutharika aliamua kujiondoa chamani humo mapema mwaka huu Lakini hata hivyo alishindwa kuunda muungano miongoni mwa makundi pinzani ya bunge na kuunda chama chake mwenyewe mwezi May cha Demokratic Progressive Party DPP ambacho hakina hata mbunge mmoja. Wa mutharika anakabiliwa na changamoto nzito kufuatia kujiondoa kwenye chama kilichomuweka madarakani. Mwaka huu rais huyo alimteua mwanamke wa kwanza kuongoza idara ya polisi nchini humo lakini uteuzi wake huo ulipingwa vikali bungeni na sasa chama kinachotawala ambacho kilimuweka madarakani yeye rais wa Mutharika UDF kinajaribu kumtoa madarakani . Mswaada wa kumtoa madarakani wa Mutharika mwezi uliopita ulishindwa kufaulu baada ya spika wa bunge kuzirai na baadae kufa na hivyo kusasabisha kuchelewa kwa kura juu ya bajeti ya mwaka 2005 na 2006 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kupata msaada wa fedha kutoka shirika la fedha la kimataifa . Msemaji wa chama cha kinachotawala nchini Malawi cha UDF Sam Mpasu amesema rais huyo amekiuka katiba ya nchi mara nyingi tangu achukue wadhifa wa urais lakini sasa chama hicho kiko tayari kumuondoa madarakani kwa kuzingatia hilo. Hata hivyo msemaji huyo hakutoa wakati maalum wa kuondolewa madarakani rais Bingu lakini aliweka bayana kwamba chama cha UDF kinaushahidi wa kutosha kuweza kumuondoa madarakani rais huyo. Malawi inaorodheshwa na benki ya dunia kuwa nafasi ya kwanza ya mataifa maskini kabisa duniani huku robo tatu ya wananchi wake wakiishi kwa dola moja kwa siku. Kwa mujibu wa mwanasayansi wa siasa Boniface Dulani rais Mutharika anaweza kuhesabiwa kufanya jambo moja tu la muhimu tangu aingie madarakani kwa kumfuta kazi waziri wake wa elimu kwa kuhusika katika ulaji rushwa. Dulani anasema wa Mutharika ni yatima wa siasa anayejaribu kutafuta uungwaji mkono miongoni mwa makundi ya kisiasa yaliyogawika nchini humo. Matatizo ya kisiasa yanayomkabili rais Bingu wa Mutharika tangu kuchukua wadhifa wa urais yameigubika kazi yake na kumsabisha kujipigania binafsi na kusahau matatizo yanayoikabili nchi kwa jumla. Dulani anasema iwapo rais huyo atashindwa kumakinika basi huenda akashindwa kutimiza ahadi alizozitoa za kuumaliza umasikini nchini humo. .

Imeripotiwa kwamba mashetani wanamfuata rais huyo akiwa katika jumba lake la kifahari kwenye ikulu ya mjini Lilongwe.

Lakini hata hivyo rais Bingu amekanusha madai hayo licha ya washauri wake wa kidini kutoa taarifa tofauti.

Rais Bingu wa Mutharika ambaye alichukua madaraka baada ya kufanyika uchaguzi uliokumbwa na utata mnamo mwaka jana hivi sasa yupo katika hali ya wasiwasi kufuatia vitisho kadha wa kadha.

Mizuka inayojitokeza katika umbo la rais wa zamani wa nchi hiyo Bakili Muluzi inadaiwa kumfuata rais Bingu na hivyo kutatiza shughuli zake za kisiasa pamoja na kuzihujumu juhudi zake za kulijenga upya taifa hilo.

Mfuasi wa Rais Bingu Agrippa Tembo ameliambia shirika la habari la Reuterskuwa hadi kufikia sasa hakuna ufadhili wowote wa kifedha uliopatikana kusaidia bajeti ya nchi.

Pamoja na hayo Malawi ni mojawapo kati ya nchi za Afrika zilizokosa nafuu ya kupunguziwa madeni,hakuna mvua angalau ya kuwezesha ukulima wa vyakula huku maradhi ya ukimwi nayo yakichukua nafasi yake nchini humo.

Alipoingia madarakani rais Bingu wa Mutharika kwanza alionekana kuwa kama kibaraka cha Muluzi, na bila kupoteza muda rais huyo alianzisha kampeini kabambe ya kupambana na rushwa akimlenga Muluzi pamoja na maswahiba zake.

Akiandamwa na vitisho vya kung'olewa madarakani kutokana na kuanzisha kamepini dhidi ya rushwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika chama cha UDF alichokuwa mwasisi mwenzi mnamo mwaka 1991,Wa Mutharika aliamua kujiondoa chamani humo mapema mwaka huu.

Lakini hata hivyo alishindwa kuunda muungano miongoni mwa makundi pinzani ya bunge na kuunda chama chake mwenyewe mwezi May cha Demokratic Progressive Party DPP ambacho hakina hata mbunge mmoja..

Wa Mutharika anakabiliwa na changamoto nzito kufuatia kujiondoa kwenye chama kilichomuweka madarakani. Mwaka huu rais huyo alimteua mwanamke wa kwanza kuiongoza idara ya polisi nchini humo lakini uteuzi wake huo ulipingwa vikali bungeni na sasa chama kinachotawala ambacho kilimuweka madarakani Mutharika UDF kinajaribu kumtoa madarakani .

Mswaada wa kumtoa madarakani wa Mutharika mwezi uliopita ulishindwa kufaulu baada ya spika wa bunge kuzirai na baadae kufa na hivyo kusasabisha kuchelewa kwa kura juu ya bajeti ya mwaka 2005 na 2006 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kupata msaada wa fedha kutoka shirika la fedha la kimataifa .

Msemaji wa chama cha kinachotawala nchini Malawi cha UDF Sam Mpasu amesema rais huyo amekiuka katiba ya nchi mara nyingi tangu achukue wadhifa wa urais lakini sasa chama hicho kiko tayari kumuondoa madarakani kwa kuzingatia hilo.

Hata hivyo msemaji huyo hakutoa wakati maalum wa kuondolewa madarakani rais Bingu lakini aliweka bayana kwamba chama cha UDF kinaushahidi wa kutosha kuweza kumuondoa madarakani rais huyo.

Malawi inaorodheshwa na benki ya dunia kuwa nafasi ya kwanza ya mataifa maskini kabisa duniani huku robo tatu ya wananchi wake wakiishi kwa dola moja kwa siku.

Kwa mujibu wa mwanasayansi wa siasa Boniface Dulani rais Mutharika anaweza kuhesabiwa kufanya jambo moja tu la muhimu tangu aingie madarakani kwa kumfuta kazi waziri wake wa elimu kwa kuhusika katika ulaji rushwa.

Dulani anasema wa Mutharika ni yatima wa siasa anayejaribu kutafuta uungwaji mkono miongoni mwa makundi ya kisiasa yaliyogawika nchini humo.

Matatizo ya kisiasa yanayomkabili rais Bingu wa Mutharika tangu kuchukua wadhifa wa urais yameigubika kazi yake na kumsabisha kujipigania binafsi na kusahau matatizo yanayoikabili nchi kwa jumla.

Dulani anasema iwapo rais huyo atashindwa kumakinika basi huenda akashindwa kutimiza ahadi alizozitoa za kuumaliza umasikini nchini humo.

.