1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mji wa Dresden upo katika tahadhari kuu ya mafuriko

18 Septemba 2024

Mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Dresden upo katika hatari ya kukabiliwa na mafuriko baada ya siku kadhaa za mvua kubwa zilizosababisha mafuriko katika maeneo mengi ya Ulaya ya Kati.

https://p.dw.com/p/4kkzo
Mafuriko barani Ulaya | Ujerumani - Dresden
Nguzo za meli za meli za Saxon zimeoshwa na mafuriko ya Elbe, kwa nyuma mandhari ya mji wa kale na Daraja la Carola lililoporomoka kwa kiasi linaweza kuonekana.Picha: Robert Michael/dpa/picture alliance

Mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Dresden upo katika hatari ya kukabiliwa na mafuriko baada ya siku kadhaa za mvua kubwa zilizosababisha mafuriko katika maeneo mengi ya Ulaya ya Kati. 

Kiwango cha maji katika Mto Elbe unaopitia mji huo wa Dresden, kimeongezeka kufikia mita 6 hali iliyoilazimisha serikali kutangaza onyo la pili kubwa la kutokea kwa mafuriko. Hii inamaanisha maeneo ya makaazi, barabara kuu, na barabara za reli zipo katika hatari hiyo ya kuzidiwa kwa maji. 

Mafuriko yasababisha madhara ikiwemo vifo barani Ulaya

Soma pia:Watu 18 wafariki dunia kutokana na mafuriko barani Ulaya 

Katika kituo cha Schöna Gauging karibu na mpaka wa Jamhuri ya Czech kiwango cha maji ya mto huo kilifikia mita 6.56 mapema hii leo asubuhi. Viwango hivyo vinatarajiwa kuendelea kupanda kabla ya kushuka wakati wa usiku.  

Hata hivyo, serikali haiamini kiwango hicho cha maji kitapita mita 7 ambayo huenda ikasababisha tahadhari kubwa zaidi kutolewa.