Mjumbe wa UM kwa Kongo atahadharisha kutanuka kwa mzozo
10 Julai 2024Katika ripoti yake aliyoiwasilisha mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Bibi Keita ametahadharisha juu ya kutanuka kwa maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa M23 kwenye mkoa Ituri kama moja ya sababu za kutia hofu.
"Kusogea kwa uwanja wa mapambano na uwepo wa silaha nzito za kivita katika maeneo yanayozunguka kambi za wasio na makaazi vinauweka rehani usalama wa watu waliokimbia mapigano na wakaazi wa maeneo hayo" Alisema Keita.
Vile vile ripoti yake imeitaja Rwanda kuwa imeongeza uungaji wake mkono kwa waasi wa M23.
Soma pia:UN: Vikosi vya Rwanda vyasaidiana na M23 kupigana Kongo
Hivi karibuni ripoti ya jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilisema zaidi ya wanajeshi 4,000 wa Rwanda wako ndani ya mipaka ya Kongo na wamekuwa wakihusika kupanga mashambulizi.