SiasaSyria
UN yaitaka Syria kurejea kwenye mazungumzo ya kisiasa
17 Machi 2024Matangazo
Mjumbe huyo ameonya kwamba mazungumzo ya kisiasa yapo "katika mwelekeo mbaya". Tangu mwaka 2019, Pedersen amekuwa akijaribu bila mafanikio kuunda kile kinachojulikana kama kamati ya katiba ya Syria, ili kuandika upya au kurekebisha katiba ya nchi iliyoharibiwa na vita.
Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa amesema hali ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi ni mbaya mno nchini Syria.
Vita vya Syria vilivyoanza miaka 13 iliyopita kwa hatua kali za kuyazima maandamano ya kuunga mkono demokrasia, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 500,000, huku mamilioni ya wengine wakiyahama makazi yao. Uchumi, miundombinu na viwanda vya nchi hiyo vimedidimia.