Mkuu wa Umoja wa Mataifa apendekeza mabadiliko ya kisera
21 Julai 2023Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterresamependekeza kuzifanyia mageuzi makubwa operesheni za kulinda amani za umoja huo akisema licha ya mafaniko yanayopatikana bado zinakabiliwa na vizingiti.
Soma pia: Umoja wa Mataifa waadhimisha miaka 75 ya walinda amani
Akiwasilisha pekendezo hilo lililopewa jina la "ajenda mpya kwa ajili ya amani" Guterres ameisifu kazi kubwa inayofanywa, ingawa amesema kuna kitisho kikubwa kinachotokana na ongezeko la mivutano ya siasa za kimaeneo, ukiukaji wa haki za binadamu na tishio linaloongezeka la vita vya nyuklia.
"Migogoro imekuwa ngumu zaidi na ni vigumu kusuluhisha. Mwaka jana kulikuwa na idadi kubwa zaidi ya vifo vilivyotokana na migogoro huku kukiibuka tena wasiwasi juu ya uwezekano wa vita vya nyuklia." Amesema Guterres.
Guterres ameomba kuwepo mabadiliko makubwa ikiwemo mipango inayokwenda na wakati na kutanua uwezo wa walinda amani kwenye uwanja wa mapigano.