Moldova yagawanyika katika kura ya maoni ya kujiunga na EU
21 Oktoba 2024Kura ya maoni nchini Moldova kuhusu iwapo katiba yake ibadilishwe na idhamirie kujiunga na Umoja wa Ulaya haijatoa mshindi wa uhakika, huku matokeo rasmi yakionyesha kura za Ndiyo na Hapana zinaenda sambamba wakati zimebakia kura chini ya 2% kuhesabiwa.
Soma: Rais wa Moldova akosoa uvamizi dhidi ya demokrasia baada ya kura ya maoni
Upande unaouunga mkono umepata kura asilimia 50.18 na upande unaopinga unakadiriwa kupata asilimia 49.92. Mpaka sasa zaidi ya asilimia 98 ya kura zimeshahesabiwa. Kulingana na utafiti wa maoni wa hadi hivi karibuni, wanaounga mkono mabadiliko walikuwa wanaongoza.
Rais aliyepo madarakani, Maia Sandu, mtetezi kubwa wa Umoja wa Ulaya, amelalamika juu ya matokeo hayo kutokana na kile alichokiita kuwa ni uingiliaji wa nchi za nje.