1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Msaidizi wa Imran Khan akamatwa kwa kukosoa uchaguzi

25 Januari 2023

Polisi nchini Pakistan imesema mshirika wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Imran Khan amekamatwa kwa makosa ya kuwakashifu maafisa wa uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4Mfh0
Indien Punjab | Imran Khan im Gespräch mit Journalisten
Picha: Talha Mehmood/PTI Media

Fawad Chaudhry, aliyekuwa waziri wa habari chini ya utawala wa Khan, alikamatwa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mjini Lahore.

Anashutumiwa kwa kuwanyanyasa na kuwatisha maafisa wa tume ya uchaguzi pamoja na familia zao katika matamshi yake hapo jana, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya polisi iliyosambazwa na chama chake cha Tehreek-e-Insaf.

Chaudhry, pia anadaiwa kuzuiliwa chini ya sheria ya uchochezi kwa sababu alijaribu kusababisha mkwamo katika mchakato wa uchaguzi.

Serikali ya Khan iliondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani mwezi Aprili mwaka 2020 baada ya washirika wake katika serikali ya muungano  kuacha kumuunga mkono.

Uchaguzi mpya unatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Oktoba huku Pakistan ikiendelea kudidimia katika mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.