Moureen ni msichana wa miaka 18 mwenye maono na ari ya kipekee, ambaye amejiweka mbele kama kiongozi katika kuhamasisha vijana kuhusu umuhimu wa elimu bora kwa maendeleo endelevu.
Anahamasisha vijana kutambua kuwa kupitia elimu, wana uwezo wa kubadilisha maisha yao na ya wengine, na hivyo kuchangia katika kujenga jamii imara na yenye ustawi.
Kipindi hiki kinakupa fursa ya kusikia ujasiri wa msichana na mchango mkubwa anaoufanya katika jamii. Msichana Jasiri ni muwazi, ana upendo na yuko tayari kujitoa kuwahudumia wengine. Ni shujaa!