Doroth ni binti aliyeandika kitabu kinachoangazia masuala muhimu yanayowahusu vijana, kama vile kujitambua, uongozi, na kufanikisha malengo ya maisha. Doroth anaamini kuwa elimu na maarifa ni nyenzo muhimu kwa kizazi cha sasa kupata taarifa sahihi. Mwandishi chipukizi Mitchelle Ceaser amekutana na Doroth kusikiliza ndoto na maono yake. Tizama na utuachie maoni.
Kipindi hiki kinakupa fursa ya kusikia ujasiri wa msichana na mchango mkubwa anaoufanya katika jamii. Msichana Jasiri ni muwazi, ana upendo na yuko tayari kujitoa kuwahudumia wengine. Ni shujaa!