Muhoozi atangaza azma ya kuchukua urais wa Uganda
28 Oktoba 2022Kulingana na wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kisiasa, ujumbe huo unaiweka Uganda katika joto la kisiasa ikiwa imesalia miaka mitatu na nusu kabla ya kuwadia msimu wa uchaguzi kuwadia.
Hapo awali, dalili za Jenerali Muhoozi kuonyesha nia yake kuwa rais wa Uganda hazikutiliwa maanani na wengi. Lakini kufuatia ujumbe wake kwenye jukwaa lake la Twitter siku ya Alhamisi ni dhahiri kwamba azma hiyo imekuwepo na anaizingatia kwa dhati. Katika ujumbe huo ametaja kuwa anataka kuwa rais wa Uganda na hilo litatokea.Museveni amuondoa mwanae ukuu wa jeshi, ampandisha cheo
Ameongezea kusema kuwa hii itakuwa ni kwa heshima ya mamake Janet Museveni ambaye katika ujumbe uliotangulia huo alimtaja kuwa malaika wake asiye na mfano. Ujumbe huu umewatumbukiza raia mbalimbali katika mjadala kuhusu nini anachopanga Jenerali Yoweri Museveni kuhusiana na urithi kwa wadhifa wa urais. Wambede Wamoto ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa ametoa mtazamo huu.
Hivi karibuni makundi mbalimbali ya vijana yameshuhudiwa yakifanya maandamano ya kumuunga Jenerali Muhoozi kuwania urais. Wao huvalia fulana na kuonyesha mabango yenye ujumbe huo wakipitia barabara za miji mbalimbali. Ijapokuwa rais Museveni mwenyewe hajataja nia yake kuwania urais mwaka 2026, bado anayo fursa hiyo kufuatia hatua ya kuondolewa kwa ukomo wa umri kwa mgombea urais nchini Uganda. Haya ni baadhi ya maoni ya vijan.
Hapo awali maafisa wa jeshi walioonyesha nia ya kushiriki siasa walichukuliwa hatua za kisheria na kufunguliwa mashtaka au kuwekwa katika vizuizi. Miongoni mwa ni Jenerali Henry Tumukunde na Sejusa. Lakini hakuna hatua za kisheria zimechukuliwa kwa jenerali Muhoozi ambaye angali afisa wa kijeshi na kwa mtazamo wa wachambuzi hii inaleta mkanganyiko katika taasisi hiyo kuhusiana na uhusika wao katika siasa za nchi. Wamoto anaongezea hivi….
Licha ya rais Museveni kumtaka mwanawe asiendelee kutumia mitandao ya kijamii kusambaza ujumbe wenye hisia za kisiasa, ujumbe huo wa hapo jana unaonyesha kuwa Jenerali Muhoozi hajazingatia ushauri wa babake. Lubega Emmanuel DW Kampala.