1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Museveni ataka kasi kuyawekea magari namba za kidijitali

16 Novemba 2023

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameagiza mpango wa utoaji wa nambari za kidigitali uharakishwe ili kusaidia katika kukabiliana na wimbi la uhalifu nchini humo. Soma na sikiliza ripoti ya Lubega Emmanuel kutoka Kampala.

https://p.dw.com/p/4YvZc

Akihutubia kwenye sherehe za kufuzu za askari polisi siku ya Jumatano, rais Museveni alichanganua mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu na ugaidi ambavyo vinazidi kuwa tishio si tu kwa maisha ya raia lakini pia mashaka kwa uchumi wa nchi.

Mataifa ya Uingereza na Marekani yalitoa tahadhari kwa kutosafiri kwenda Uganda, waliopo ndani ya nchi hiyo wawe makini na nyendo zao kutokana na hali dhaifu ya usalama.

Miongoni mwa njia ambazo Museveni anasisitiza zifuatwe ni kuharakisha ule mpango wa magari yote kuwa na nambari za kidigitali ili ppopote pale gari lilipo, serikali na vyombo vya usalama vinaweza kufuatilia mienendo ya watu waliomo.

Mpango wa namba za kidijitali wakosolewa


Hata hivyo, hatua hiyo ya kutaka magari kuwa na nambari za kidigitali iliyoazinduliwa wiki iliyopita na waziri wa uchukuzi kandarasi ikipewa kamuni moja ya urusi, imekosolewa na Shirika la Kimataifa linalofuatilia hali za binadamu Human rights watch.

Uganda Kampala | Polisi wakishika doria baada ya tukio la kihalifu
Wasiwasi wa usalama umeongezeka nchini Uganda katika siku za karibuni Picha: Hajarah Nalwadda/AP/picture alliance

Shirika hilo linasema hii itakuwa hatari kubwa kwa haki za watu kwani maisha yao yatafuatiliwa na pia yaweza kutumiwa kuwaandama wapinzani wa serikali badala ya kuzingatia masuala ya usalama wa nchi. 


Raia mbalimbali pia wamelezea mashaka yao kuhusu mpango huo wakisema kuwa ni njia nyengine ya serikali kukusanya mapato kwani mpango huo ukitekelezwa utaingizia serikali shilingi dola mia mbili hivi kutoka kwa gari moja na dola hamsini kutoka kwa mmiliki wa pikipiki. 


Wakati huohuo, Uganda imetangaza kuimairisha usalama kwenye mipaka yake na jamhuri ya kidemokrasia ya congo kufuatia mashambulizi ya raia katika vijiji vinavyopakana na wilaya ya bundibugyo.

Hadi sasa zaidi ya wakimbizi 2,000 wa DRC wameingia Uganda katika muda wa siku mbili kufuatia mashambulizi hayo.